Makonda aitabiria ushindi Simba Uwanja wa Taifa leo


By Charity James
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba kuendelea kulinda rekodi yao ya kutokufungwa mchezo hata mmoja na kutoa aibu ya kufungwa mbele ya Rais Joseph Magufuli
Simba inatarajia kushuka dimbani leo kuumana na Kagera Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa nane mchana.
Makonda alisema alisema uwepo wa Rais Magufuli katika dimba la Taifa ni jambo moja kubwa sana kutokea kwa sababu tangu awe mkuu wa mkoa na serikali ya awamu tano kuingia madarakani halijawahi kufanyika suala kama hilo.
"Nina timu nyingi katika mkoa wa Dar es Salaam ambazo zimeshiriki katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara lakini tunafahamu sote kwamba Simba SC anakwenda kukabidhiwa kikombe kwa hiyo nikiwa kama Mkuu wa Mkoa huu na kombe kubakia hapa ni furaha kubwa na fahari kwa wananchi wa Jiji hili", alisema Makonda.
"Haitakuwa jambo jema tunakabidhiwa kombe halafu tukafungwa na watu Kagera Sugar hapana, mimi nina imani pia ndugu zangu wakina Emmanuel Okwi watatupa burudani ya kuendeleza heshima yetu ya kuchukuwa ubingwa bila ya kufungwa. Pia niwahakikishie usalama wa kutosha mwanzo wa mechi na hadi mwisho itakapomalizika".
Timu ya Simba imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuwa na alama 68 kwenye mechi 28 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga yenye alama 48 kwenye mechi 26.


Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment