Mafisango amliza Kichuya, Kapombe


By Olipa Assa
Mwaka 2012, Simba ilipochukua ubingwa, kati ya wachezaji muhimu waliosababisha mafanikio hayo ni  Patrick Mutesa Mafisango na ndio jambo ililowapelekea mastaa wa timu hiyo kunena haya. 
Kutokana na mafanikio ambayo Simba, wameyapata kwa msimu huu, yamewafanya nyota wa timu hiyo, kumzungumzia Mafisango na kwamba kama anaona huko alipo basi atakuwa amepata faraja iliyokosekana ndani ya miaka mitano.
Winga wa timu hiyo, Shiza Kichuya alitoa la moyoni akisema: " Jina la Mafisango ni ngumu kufutika moyoni mwangu, kwani ni kati ya wachezaji ambao nilikuwa nawakubali ufundi wao wa uwanjani, hivyo ubingwa tuliochukua ni faraja."
"Kitu pekee cha kumuenzi ni kujituma na kuonyesha uwezo kama alivyokuwa anafanya yeye akiwa uwanjani, kwa wale ambao ni wafuatiliaji wa soka, wanatambua jinsi jamaa alivyokuwa anateleza na mpira," alisema Kichuya.
Kichuya anasema, kabla ya kuchukua ubingwa alikuwa anapenda kwenda kushangilia kwenye picha ya Mafisango, kuonyesha jinsi ambavyo anaguswa juu ya jambo hilo na kwamba ubingwa walioupata anaona umeenzi kazi ya marehemu.
"Nikiwa nje ya Simba, wapo wachezaji ambao nilikuwa nawapenda akiwemo Mafisango, ila mwisho wa siku kila binadamu anapita, ninachoweza kusema, apumzike kwa amani kaka yetu,"anasema.
Shomary Kapombe ni kati ya wachezaji ambao walikuwepo katika kikosi ambacho kilichukua ubingwa mwaka 2012 wakiwa na marehemu Mafisango, amezungumzia namna alivyomkumbuka katika mafanikio hayo.
 "Mafisango alikuwa anajua anachokifanya uwanjani, alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania, katika ubingwa huu, namkumbuka kwa mengi, kikubwa Mungu ampumzishe kwa amani,"anasema.

Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment