Makonda ashangazwa suala la Uwanja wa Ndani wa Taifa



By Thomas Ng'itu
Dar es Salaam: Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam, Paul Makonda, ameshangaa kusikia kwamba vifaa alivyotoa kukarabati wa Uwanja wa Ndani wa Taifa (indoor), unaotumika kwa ajili ya michezo wa Mpira wa Netball na Basketball  havijatumika ipasavyo.
Makonda amesema, vifaa hivyo alikabidhi vyote na vilipokelewa, hivyo kama havijafanyiwa kazi ni jambo linalomshangaza.
"Niliahidi kupeleka jenereta, mipira na mabati nikafanya hivyo na nilitoa mpaka pesa za ukarabati kama hawajatengeneza ndio nasikia hivi sasa lakini nitalifanyia kazi.  Jenereta lile nilipewa mimi kwa ajili ya nyumbani kwangu lakini niliamua kupeleka kule badala ya kulitumia," anasema Makonda.
Makonda ameongeza kwamba atawasiliana na viongozi na kutuma vijana wake ili waweze kuhakikisha uwanja huo unafanyiwa ukarabati.
Kiongozi huyo aliwahi kuahidi kwamba atafanya marekebisho katika uwanja huo wa mpira wa pete, lakin bado haijaonekana kuwepo kwa  kiwango cha mabadilisho ilihali vifaa vilitolewa.

Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment