Nyota Kagera Sugar wapania kutibua sherehe za Simba



By Masoud Masasi
Mwanza. Kagera Sugar inatarajia kuwavaa Simba kesho Jumamosi, huku nyota wa kikosi hicho tamba kuwa wamejipanga kutibua sherehe yao kwa kuhakikisha wanawafunga katika mpambano huo wa Ligi Kuu.
Simba ambao ni Bingwa mpya wa Ligi Kuu msimu huu, wanatarajiwa kukabidhiwa Kombe lao baada ya mchezo huo kumalizika.
Nyota wa Kagera Sugar walisema kuwa licha ya kwamba wapinzani wao wameshatwaa Ubingwa, lakini watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwatibulia sherehe yao.
Nahodha wa timu hiyo, George Kavila alisema kuwa wamejiandaa vyema kuhakikisha wanapambana kusaka ushindi ili kujihimarisha vyema kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Alisema kuwa licha ya kwamba nao wameshajihakikishia kubaki kwenye Ligi msimu ujao kwa pointi zao 31, lakini wanahitaji alama tatu nyingine ili kupanda nafasi za juu.
“Ni mchezo mgumu kutokana na umuhimu wa ushindi kwa timu zote,lakini sisi tumejiandaa vizuri na nia yetu ni kumaliza Ligi katika nafasi nzuri,” alisema Kavila.
Naye Christopher Edward alisema kuwa Simba isitarajie mteremko katika mchezo huo na kwamba lazima wawatibulie rekodi yao ya kutokufungwa hadi sasa.
“Hiyo rekodi inaweza kuvunjwa,tumejipanga vizuri na niwaambie tu kuwa wasitarajie mteremko,lazima tuwatibulie”alitamba Edo huyo aliyewahi kukipiga kwa Wekundu hao.
Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa kikosi hicho,Ally Jangalu alisema kuwa kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya mtanange huo na kwamba ambapo amesema hawana majeruhi wowote.


Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment