Makonda awahakikishia Simba usalama


By Thomas Ng'itu
Kuelekea mchezo wa kesho wa Simba na Kagera Sugar,  Paul Makonda ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam, amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kushuhudia Wekundu wa Msimbazi wakikabidhiwa kombe lao la  Ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku akisisitizia ulinzi wa kutosha utakuwepo.
Makonda amesema, mashabiki wasiwe na wasiwasi katika suala la ulinzi na wote wote watakaokwenda uwanjani hapo watakuwa salama kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli atakuwepo.
"Hakutakuwa na tatizo lolote kwasababu mkuu wa nchi atakuwepo pale hivyo ulinzi utakuwa wa kutosha na kila mmoja atawahi kwenda nyumbani kupata iftari," amesema.
Wakati huo huo Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka na kusema kuwa imewabidi wapunguze gharama ya viingilio ili mashabiki wao waweze kupata nafasi ya kufika uwanjani.
"Kesho watu waje wakiwa wamevaa jezi zilizoandikwa Simba bingwa, lakini pia kiingilio cha chini ni shilingi elfu mbili hivyo naamini kabisa kwamba kila shabiki ataweza kuingia,"alisema.

Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment