Kocha Mkongo atimka Yanga



By Mwandishi Wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera anaondoka jioni ya leo Ijumaa, kwenda kwao Congo kwa ajili ya kujiunga na timu yake ya taifa inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia.
Zahera anakwenda Congo kutokana na makubaliano maalumu waliyofanya na Yanga kuwa pamoja na kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani, hataacha majukumu kwenye kikosi chake cha timu ya taifa.
"Mwalimu ataandoka jioni hii kwenda kujiunga na timu yao ya taifa na baada ya mchezo huo atarudi kuungana na Yanga,"amesema kiongozi wa Yanga.
Kutokana na kuondoka kwake, Yanga ambayo inajiandaa na mechi ya ligi kuu dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage itabaki chini ya makocha wasaidizi, Shadrack Nsajigwa na Mzambia Noel Mwandila watakiongoza kikosi hicho.


Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment