Okwi, Bocco uso kwa uso na Walcott


By ELIYA SOLOMON
SIMBA awamu hii haitaki masikhara kabisa. Unaambiwa jana Alhamisi mashindano ya Kombe la SportPesa yalizinduliwa rasmi ambapo bingwa wake atatua jijini Liverpool kukipiga na Everton ya Theo Walcott.
Sasa mabosi wa Simba fasta tu wakachukua simu na kuwaambia nyota wao kuwa kuna fedha ndefu zinawahusu endapo watakamilisha kazi hiyo.
Mbali ya kwenda kucheza Everton ambayo staa wa zamani wa Arsenal, Walcott na nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney wanaichezea, bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa Dola 30,000 (Sh 68 milioni).
Mabosi wa Simba ambao wametumia zaidi ya Sh3 bilioni msimu huu, wamewaambia nyota wao wakiwamo Emmanuel Okwi na John Bocco waliofunga mabao 34 Ligi Kuu Bara, kuwa wakitwaa taji hilo watagawana zawadi hiyo kwani wao wanataka heshima ya kwenda England kukipiga na watani hao wa jadi wa Liverpool.
Mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Juni 3 hadi 10 nchini Kenya, yatahusisha timu za Simba, Yanga, Singida United na JKU ya Zanzibar kutoka Tanzania.
Nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni za wenyeji Kenya ambazo ni Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys. Wawakilishi wa Simba na Yanga, Said Tully na Charles Mkwassa, walithibitisha kuwa lazima wapeleke nyota wao wote tofauti na msimu uliopita ambapo, walichezesha timu za vijana.
“Kama timu tumejiandaa na tupo tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba na Tanzania kwa ujumla. Tutakwenda na kikosi kamili ili kuendeleza ubabe kama tulivyofanya msimu huu kwenye ligi,” alisema Tully aliyeongozana na Ofisa Habari wao, Haji Manara.
Naye Manara alisema: “Fedha za ubingwa zitakwenda kwa wachezaji endapo wataifanya kazi hiyo kwa ukamilifu. Tunataka heshima, pesa watagawana.”
Kwa upande wake Mkwasa alisema: “Tulikuwa tukisumbuliwa na majeraha kwa baadhi ya wachezaji muhimu ndio maana tuliteleza, hii ni nafasi nyingine kwenda kutwaa ubingwa huo ili tucheze na Everton.”
Mbali ya bingwa kujizolea dola 30, 000, timu zitakazoshika nafasi ya pili na tatu zitapata kifuta jasho cha dola 7,500 na dola 5,000 (Sh16 milioni na Sh 11 milioni). Kabla ya mashindano hayo kila timu itapewa dola 10,000 (Sh22 milioni) kwa ajili ya maandalizi.
Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment