Manara ajitosa kuwalipia kiingilio wasio na mkwanja Taifa



Dar es Salaam. Wakati amshaamsha ya mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa kesho Jumamosi ikiendelea kila kona,  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameweka wazi kwamba atajitolea kuwalipia mashabiki kiingilio.

Manara ametoa kaulio hiyo kwenye mahojiano katika kipindi cha Sport HQ kilichorushwa leo Ijumaa asubuhi, ikiwa ni maandalizi ya mechi yao ambayo pia itahudhuriwa na Rais Dk John Magufuli.

Manara alisema atawalipia  baadhi  tu ambao watakuwa hawana pesa ya kiingilio na atakuwepo getini tayari kuwagawia Sh 2000 walengwa.
Simba inatarajiwa kukabidhiwa Taji lao la ubingwa kesho wakati Rais Magufuli atakuwa akiwapokea vijana wa Serengeti Boys ambao walitwaa ubingwa wa CECAFA.


Share on Google Plus

About Chagaboy

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment